Mwezi tano Safar bibi Ruqayyah binti wa Imamu Hassan (a.s) afariki dunia

Maoni katika picha
Wapenzi na wafuasi wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) wanasema kuwa mwezi tano Safar, ni siku ya msiba mkubwa usioelezeka, unaumiza moyo sana kabla ya macho kutoa machozi, msiba wa kifo cha bibi Ruqayyah mtoto wa Hussein (a.s), ni machungu makubwa mno kutaja kifo chake.

Bibi Ruqayyah (a.s) alikua na umri wa miaka mitatu katika tukio la Karbala, aliona kwa macho yake kila kilicho tokea Karbala, hadi kuuawa kwa baba yake Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, kisha alichukuliwa mateka pamoja na watu wengine wa nyumba ya Mtume (a.s) hadi Kufa, kisha wakapelekwa Sham.

Walipokua Sham Yazidi aliamuru wawekwe katika moja ya jela zake, siku moja akaamka usiku, akashtuka kutoka usingizini na akasema: yuko wapi baba yangu Hussein? Mimi nimemuona usingizini, wakima mama walipo sikia hivyo wakalia, na watoto wote wakalia, sauti za vilio zikawa kubwa.

Yazidi (laana iwe juu yake) akaamka kutoka usingizini, akasema: kuna habari gani? Wakamuambia kilicho tokea, akaamuru apelekewe kichwa cha baba yake, wakamletea kichwa kitakatifu kikiwa kimefunikwa kitambaa, akawekewa mbele yake, walipo funua kitambaa akaona ni kichwa kitakatifu, akaita (Ewe baba yangu nani amemwaga damu yako? Ewe baba yangu nani amekata shingo yako? Ewe baba yangu nani kanifanya kuwa yatima katika umri mdogo? Ewe baba yangu nani tumtegemee baada yako? Ewe baba yangu nani atalea mayatima hadi tuwe wakubwa)?

Kisha akaweka mdomo wake juu ya mdomo wa baba yake mtukufu, akalia sana hadi akazimia, walipo mtikisa wakakuta tayali amefariki, vilio vikaongezeka, kila mtu alilia siku hiyo.

Ilikua ni siku ya mwezi tano Safar (61h), akazikwa sehemu alipofia akiwa na miaka mitatu au minne, au zaidi ya hapo kidogo -kutokana na tofauti za riwaya- kaburi lake lipo umbali wa mita mia moja au zaidi kutoka msikiti wa Umawiyyu katika mji mkuu wa Damaskas kwenye mlango wa Faradiis, nao ni mlango mashuhuri na mkongwe katika mji huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: