Baina ya haram mbili imepangwa foleni ndefu zaidi ya chakula kwa jina la bibi Ruqayya

Maoni katika picha
Eneo la katikati ya haram mbili tukufu jioni ya jana siku ya Jumapili (4 Safar 1443h) sawa na tarehe (12 septemba 2021m) imepangwa foleni ndefu zaidi ya chakula kwa jina la bibi Ruqayya mtoto wa Hussein (a.s), katika kumbukumbu ya kifo chake kwa huzuni na majonzi makubwa.

Maombolezo haya yanafanywa kwa mwaka wa kumi chini ya usimamizi wa umoja wa kimataifa wa watumishi wa bibi Ruqayya (a.s) kwa kushirikiana na kitengo kinacho hudumia uwanja wa katikati ya Ataba mbili tukufu na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, imekua kawaida kwa watu wa Karbala kufanya maombolezo haya wakishirikiana na mazuwaru wa malalo mbili takatifu.

Program ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo somwa na bwana Mustwafa Swarraaf, ikafuatia ziara ya bibi Ruqayya (a.s) iliyosomwa na Muhammad Ridhwa, kisha Sayyid Mustwafa Twawirijawi akasoma maswaibu yaliyo amsha huzuni za msiba na kuliza watu.

Halafu washairi mbalimbali walipanda kwenye mimbari na kusoma mashairi ya huzuni na kuomboleza msiba wa bibi Ruqayya, mwisho wa program hii likafanywa igizo lililo onyesha baadhi ya mazingira ya kifo kilicho tokea mwezi tano Safar baada ya mateka kuwasiri Sham na kuonyesha mazingira yaliyopelekea kufariki bibi Ruqayya (a.s).

Chakula cha maombolezo kimewekwa juu ya busati la kijani liliwekwa miba, inayo ashiria shahidi huyo mdogo namna alivyo kua anatembea juu ya miba siku ya Ashura, halafu kuna kandili zilizo washwa na mishumaa, aidha wamewekwa watoto wenye jina la Ruqayya (a.s) na waombolezaji wanaomba haja zao kwa kutabaruku na chakula hicho, hususan wanawake na watoto.

Kifo cha bibi Ruqayya (a.s) ni miongoni mwa visa vya kuhuzunisha sana katika historia, kwani ndiye Hashimiyya wa kwanza kufariki baada ya kuuawa Imamu Hussein (a.s) akiwa na miaka mitatu au minne kutokana na tofauti za kihistoria.

Hakika bibi Ruqayya (a.s) alimuona baba yake katika usingizi, akaamka akiwa anamtafuta huku analia, maluuni Yazidi bun Muawiya akamsikia, akaagiza apelekewe kichwa cha baba yake, alipo funuliwa kichwa cha baba yake, akakikumbatia na akalia hadi akafa, akawa mateka wa kwanza kufariki kwa majonzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: