Idara ya Qur’ani inaendesha shindano la kuhifadhi khutuba mashuhuri ya bibi Zainabu (a.s) aliyotoa katika majlisi ya Yazidi.
Kiongozi wa Idara hiyo bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema: “Kutokana na ukubwa wa jambo hili tumeruhusu ushiriki wa wanawake wa rika zote, majina ya washindi yatatangazwa mwezi wa Rabiul-Awwal kupitia mtandao wa idara ya Qur’ani wa facebook”.
Akasema: “Ushiriki wa shindano hili unafanywa kwa kujisajili kupitia anuani (alwahdaalqurania@) na mshiriki ataje taarifa zifuatazo: (Majina matatu, umri, mkoa, namba ya simu, kiwango cha elimu yake)”, akaongeza kuwa: “Baada ya hapo atapigiwa simu ya video na wakina dada wanao simamia shindano hilo na kusoma moja kwa moja khutuba hiyo”.
Akakumbusha kuwa: “Wataanza kupigiwa simu mwezi (21 Safar) hadi mwisho wa mwezi, khuduba ihifadhiwe kama ilivyo andikwa katika kitabu cha (Luhuufu fii qatla tufuuf)”, akasema kuwa: “Kutakua na zawadi kwa washindi wa shindano hili”.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na idara kupitia ukurasa wake wa facebook.