Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza majina ya walioshinda kwenye shindano la Muraqi Almujtaba la mashairi awamu ya kwanza

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya Jumatatu, ilitangaza majina ya washairi walioshinda kwenye shindano la Muraqi Almujtaba (a.s) la mashairi, katika hafla iliyofanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo (Imamu Mujtaba ni wasii mkarimu na njia Madhubuti).

Hafla ya kutoa zawadi kwa washindi imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya na katibu mkuu pamoja na baadhi ya viongozi wa Ataba, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ukafuata ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na makamo kiongozi mkuu wa taaluma katika chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Alaa Mussawi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika kazi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya chini ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi katika sekta ya uandishi na uchapishaji wa vitabu, inasaidia kujibu dhulma aliyofanyiwa Imamu Hassan (a.s).

Akaongeza kuwa: “Chuo kikuu cha Al-Ameed kimekua mstari wa mbele daima katika kunusuru na kueleza mambo yanayo husu Maimamu watakatifu hususan Imamu Hassan (a.s), na nyie mnatambua kuwa historia ya umma huandikwa kwa kaswida za washairi, historia ya waarabu iliandikwa kupitia tungo za washairi, leo tunawataja washairi walio saidia kuondoa dhulma aliyofanyiwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s)”.

Halafu mashairi yaliyoshinda yakaanza kusomwa mbele ya wahudhuriaji, kama ifuatavyo:

Mshindi wa kwanza: kaswida (hawakutambua kioo) ya mshairi Naaswir Zaini kutoka Baharair.

Mshindi wa pili: kaswida (kwa heshima ya mwanga) ya mshairi Khaliil Akaari Rasni Gharbawi kutoka Iraq.

Mshindi wa tatu: kaswida (mizani ya mwanga) ya mshairi Mudhwiru Abdulmajidi Alusi kutoka Iraq.

Mshindi wa nne: kaswida (ufunguo wa mlango wa Naharaat) ya mshairi Khalidi Abdurahmani Hassan kutoka Iraq.

Mshindi wa tano: kaswida (kufunua mbele ya Mujtaba) ya mshairi Haidari Ahmadi Abduswaahibu kutika Iraq.

Mshindi wa sita kaswida: (kamavile mimi ni hudihudi narudu kutoka kwa Hassan) ya mshairi Ahmadi Alawi kutoka Baharairi.

Mshindi wa saba kaswida: (safari katika kivuli cha kanzu yake) ya mshairi Hassan Ali Rahifu kutoka Iraq.

Mshindi wa nane: kaswida (safari ya fani ya udongo) ya mshairi Muhammad Baaqir Ahmadi Jaabir kutoka Lebanon.

Mshindi wa tisa: kaswida (Haatamu bun Haashim) ya mshairi Masaar Riyaadh kutoka Iraq.

Mshindi wa kumi: kaswida (Hakika tumefungua) ya mshairi Liith Ali Taufiq Hassan kutoka Iraq.

Kuna kaswida zingine saba ambayo waandishi wake wamepewa zawadi ambazo ni:

  • - Kaswida (subhana hii huzuni) ya mshairi Ali Hassan Naaswir kutoka Saudia.
  • - Kaswida (jicho la ghaibu) ya mshairi Hamza Hussein Abbadi kutoka Iraq.
  • - Kaswida (kukiri kwa nukuu za kihistoria) ya mshairi Ali Najmu Abdullahi kutoka Iraq.
  • - Kaswida (karibu na Ghadiir tukufu) ya mshairi Dokta Ahmadi Jaasim Muslim Alkhiyaali kutoka Iraq.
  • - Kaswida (tumezinywesha nafsi zao) ya mshairi Hassan Sami Abdullahi kutoka Iraq.
  • - Kaswida (mkulima wa ngano) ya mshairi Hamida Qassim Bandari Askari kutoka Iraq.
  • - Kaswida (sababu ya mwisho ya kushushwa) ya mshairi Ali Makkiy Shekhe kutoka Saudia.

Ukafuata ujumbe wa kamati ya majaji ulio wasilishwa na Dokta Ahmadi Alyawi, akabainisha vigezo walivyo tumia katika kushindanisha kaswida zilizo shiriki, hafla ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi washindi na kila aliyechangia kufanikiwa shindano hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: