Wazee na vijana: Naswiriyya yajitokeza kupokea mazuwaru wa Arubaini na kuwahudumia

Maoni katika picha
Njia zinazo tumiwa na mazuwaru katika mkoa wa Dhiqaar na makao makuu yake Naswiriyya zinashuhudia makundi makubwa ya mazuwaru wa Arubaini, alfajri ya leo siku ya Jumanne (6 Safar) misafara mingi ya mazuwaru inapita.

Ripota wa Alkafeel ambaye yupo kwenye misafara hiyo amesema: “Njia za mazuwaru katika mji wa Fuhudi zipo aina mbili, kwamza zinaelekea katika mji wa Twaar, zipo njia mbili, ya kwanza njia ya Aalu Juwaibir -Akikah, na pili ya Twaar Karama bani Asadi- soko la wazee (Suuq shuyuukh), njia za pili zinaelekea Sayyid Dujail, watu huchagua moja ya njia hizo”.

Akaongeza kuwa: “Barabara zote kubwa na ndogo zimejengwa mabanda ya mawakibu za kutoa huduma, sambamba na nyumba zilizo fungua milango kwa ajili ya kupokea mazuwaru watukufu na kuwapa huduma zote zinazo hitajika”.

Tambua kuwa barabara hizo katika siku za kawaida huwa hazina watu wengi, lakini hivi sasa zinamsongamano mkubwa wa watu, watoa huduma wamesema kesho au keshokutwa watamaliza kazi katika barabara hizo, watafunga maukibu zao na kuelekea Karbala kufanya ziara.

Tunakuletea sehemu ya picha za mazuwaru..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: