Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Maj’maa Ilmul-Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha mihadhara katika maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Baabil katika mwezi wa Muharam na Safar.
Sambamba na kufundisha harakati ya Imamu Hussein kwa kuilinganisha na Qur’ani tukufu, na nafasi yake katika kujenga jamii, mihadhara hiyo imepata muitikio mkubwa wa vijana na mabinti.
Viongozi mbalimbali wa hauza wanashiriki kwenye program hiyo tukufu kwa kutoa mafundisho yatokanayo na vizito viwili.
Tambua kuwa program inalenga kutoa mafunzo ya Dini tukufu ya kiislamu katika jamii, jambo hilo linafanywa na tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu, kutokana na athari nzuri inayopatikana katika nyoyo za waumini.
Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati tofauti za Qur’ani tukufu, sambamba na semina endelevu za Qur’ani na harakati zingine.