Zaidi ya watu laki moja na elfu sabini na tano wamefanyiwa ziara kwa niaba katika mwezi wa Muharam na maandalizi yanaendelea ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya taaluma na mitandao chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa, dirisha la ziara kwa niaba la mtandao wa kimataifa Alkafeel katika toghuti rasmi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limefanya ziara (175,648) kwa niaba ya watu wa ndani na nje ya Iraq katika mwezi wa Muharam.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: “Mwezi wa Muharam tuliweka utaratibu maalum wa kufanya ziara hizo, tunamshukuru Mwenyezi Mungu, tulifanikiwa kupokea maombi mengi na wote tumewafanyia ziara, kama ifuatavyo:

  • - Ziara ya Ashura makhsusi.
  • - Ziara ya kila siku ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), nayo ilisombwa siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam.
  • - Ziara ya kila siku katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Ziara ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s) katika mji wa Madina wakati wa kumbukumbu ya kifo chake.
  • - Ziara ya siku za Ijumaa ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akabainisha kuwa: “Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndio waliosimamia ufanyaji wa ziara hizo, ispokua ziara ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s), imefanywa na watu waliojitolea wanaoishi Madina nchini Saudia, wamefanya ziara na kuswali rakaa mbili za ziara na kusoma dua pamoja na ibada zingine”.

Akafafanua kuwa: “Dirisha la ziara kwa niaba limepokea maombi mengi kutokana na mazingira ambayo dunia inapitia kwa sasa pamoja na Iraq, idadi kubwa ya watu hawawezi kusafiri na kuja kufanya ziara wenyewe, maandalizi yanaendelea ya ziara ya Arubaini”.

Akamaliza kwa kusema: “Asilimia kubwa ya watu waliojiandikisha wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistani, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Sweden, Kanada, Kuwait, Malezia, Australia, Aljeria, Baharaini, Misri, Ujerumani, Island, Namsa, Yunani, Holandi, Tunisia, Denmak, Norwey, Qatar, Ubelgiji, Moroko, Afghanistani, Omani, Ekwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijani, Qabras, Finland, China, Ailend, Honkon, Japani, Falme za kiarabu, Sudani)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: