Mji wa Basra umekua mtupu na mji wa Naswiriyya wafurika watu wanaotembea kwenda kufanya zaira ya Arubaini

Maoni katika picha
Mji wa Dhiqaar umefurika watu wanaotembea kwa miguu kutoka katika mji wa Basra wakielekea katika ardhi ya uhuru na utukufu (Karbala), mji wa Basra umekua mtupu baada ya watu kuanza kuondoka katika mji huo kwa zaidi ya siku saba sasa.

Sehemu ya mawakibu za kutoa huduma katika mji wa Basra zimeenda katika mikoa mingine inayopitiwa na mazuwaru, huku maukibu zingine zikifunga kutoa huduma na kusubiri msimu ujao, mawakibu zingine zimeenda kutoa huduma Karbala na kushiriki kwenye maombolezo.

Akaongeza kuwa: “Kwa mujibu wa taarifa ya ripota wa mtandao wa Alkafeel, misafara ya mazuwaru imefika kilele chake katika mkoa wa Dhiqaar hususan barabara zinazo pakana na mkoa wa Muthana, mikoa hiyo inapitiwa na mazuwaru wengi wanaoenda Karbala, na idadi ya maukibu za kutoa huduma inaendelea kuongezeka siku baada ya siku, wanatoa huduma mbalimbali kwa kiwango kikubwa”.

Aidha mazuwaru wanaendelea kumiminika kutoka mkoa wa Misaan wakielekea upande wa Diwaniyya, ambako wataenda hadi mji wa Hilla wakipitia wilaya ya Qassim, au mji wa Najafu kisha wanatembea hadi Karbala.

Hakuna kitu kinacho wasumuka kufanya kazi na kutoa mali ispokua mapenzi ya Hussein (a.s), mazingira ya kila mtu yanaonyesha kauli isemayo:

Labbaika, kama haukupata watu wa kuitika wito wako na kuja kukunusuru, hakika moyo wangu ulikujibu na masikio yangu na macho yangu.

Zifuatazo ni sehemu ya picha za misafara ya mazuwaru..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: