Kitu gani kilisemwa na kichwa cha mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) kumuambia muovu wa zama zake?

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa msafara wa mateka wa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) ulipo wasiri katika Qasri la Yazidi -laana iwe juu yake-, aliamuru nyumba yake ipambwe na akawekewa kitanda kilicho wekwa glasi za dhahabu na fedha pembeni yake, Yazidi akakaa kwenye kitanda hicho akiwa kavaa taji lililotengenezwa kwa duri na yaquut, mbele yake akiwa na watu mia nne katika watumishi wake na mabalozi wa wafalme wa kikristo na wengineo, na wazee wa kikuraishi.

Yazidi akaagiza kichwa cha Hussein (a.s), kikawekwa mbele yake kikiwa kwenye sahani ya dhahabu, wanawake walikua wamekaa nyuma yake, Sukaina na Fatuma wakawa wanamuangalia, walipo ona (kichwa cha Hussein a.s) wakaanza kulia.

Yazidi akaamuru waingie ndani, kisha akachukua fimbo yake na akaanza kukichoma choma huku anasema:

Leo nimelipiza kisasi cha siku ya Badri. Akasema maneno ya Haswiin bun Himaam:

Watu wetu walikataa kutusifu, basi nawasifu nikiwa na fimbo mkononi inayovuja damu.

Tunakata vichwa vya watu muhimu waliokua waovu na madhalimu.

Akasema Yahaya bun Hakam bun Aaswi ndugu wa Marwani alikua amekaa mbele yake:

Vichwa vya waliolala Twafu vinaukaribu zaidi ya ibun Ziyadi mja mwenye vitimbi.

Jana imetajwa nasabu yake leo familia ya Mtume hawana tena nasabu.

Yazidi akampiga mgongoni na kumuambia: Nyamaza huna mama wewe.

Abuu Barza Aslamiy anasema: Nashuhudia kuwa nilimuona Mtume anabusu mdomo wake na mdomo ya kaka yake Hassan (a.s) huku akiwaambia: “Nyie ni mabwana wa vijana wa peponi, mwenyezi Mungu awalaani watakao kuuweni, awaandalie jahanama mafikio maovu”. Yazidi akakasirika na akaamuru atolewe kwa nguvu.

Mjumbe wa Qaisar akamgeukia Yazidi na kusema: katika baadhi ya visiwa kuna kwato ya ngamia wa Issa, sisi huenda kufaya ziara huko kila mwaka na tunaitukuza sana kama mnavyo tukuza kitabu chenu, nashuhudia kuwa mko katika batili!! Yazidi akachukia kwa maneno hayo na akaamuru auliwe, akaende kubusu kichwa na akatoa shahada, wakati alipokua anauliwa, watu wakasikia sauti kubwa ikitoka kwenye kichwa kitakatifu isemayo “Laa haula walaa quwata illa billahi” kisha kichwa kilitolewa na kuwekwa kwenye mlango wa qasri kwa muda wa siku tatu
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: