Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kilichotokea tarehe saba ya mwezi wa Safar, majlisi ya kuomboleza imefanywa ndani ya ukumbi wa kitivo cha uhandisi, imehudhuriwa na wakufunzi na watumishi.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na muhadhara wa Shekh Jafari Waailiy, uliohusu historia ya Imamu Almujtaba (a.s), na kazi kubwa aliyofanya katika kusambaza elimu ya kiislamu, akaeleza mambo aliyofanya ndani ya miaka kumi aliyokaa Madina (baada ya kifo cha baba yake a.s), hususan katika sekta ya elimu ya Dini na kukamilisha safari ya babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na baba yake kiongozi wa waumini (a.s), sambamba na kueleza nafasi yake mbele ya babu yake (s.a.w.w), akaeleza pia dhulma aliyofanyiwa na watawala wa zama zake hadi akafikia kuuawa kwa sumu.
Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kinazingatia uhuishaji wa matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), sawa yawe ya kuzaliwa au kufariki, huadhimisha kila tukio kulingana na mazingira ya tukio husika.