Misafara ya mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) yamiminika katika mji wa Muthanna na wakazi wa mji huo wajitokeza kuwahudumia

Maoni katika picha
Asubuhi ya Ijumaa mwezi (9 Safar 1443h) sawa na tarehe (17 Septemba 2021m) misafara ya mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) kutoka kusini mwa Iraq imewasiri katika mkoa wa Muthanna na makao makuu yake Samawah, baada ya kumiminika katika barabara zinazoelekea upande wa Batwihaa, uliopo upande wa kaskazini umbali wa (klm 45) na kutoka katika mji wa Muthanna kama (klm 70).

Ripota wa mtandao wa Alkafeel ambaye yupo katika matembezi hayo amesema: “Misafara ya mazuwaru wanaotumia barabara za Naswiriyya imewasiri katika kitongoji cha Batwihaa upande wa mji wa (Daraji) hadi katika mipaka ya mkoa wa Muthanna katika eneo la (Hawaishali) wilaya ya Khadhar”.

Akaongeza kuwa: “Mawakibu za kutoa huduma katika mji wa Naswiriyya zinaendelea kupokea mazuwaru kwa wingi, baadhi ya mawakibu zinaendelea kutoa huduma, zingine zimeanza kufunga utoaji wa huduma na zingine zimeenda kutoa huduma katika mkoa wa Karbala na kufanya maombolezo, kawaida hapa mkoani mazuwaru watapungua katika mkoa huu hivi karibuni”.

Akabainisha kuwa: “Kila mtu anaeingia katika ardhi ya Muthanna, anakuta wakazi wa mji huo na mawakibu zao wako tayali kumuhudumia, bali wanaingia barabarani na kuwakaribisha, huu ni utamaduni walio rithishana kizazi na kizazi”.

Mazuwaru wameendelea kumiminika kwa wingi wakitokea mkoa wa Misaan na kuelekea mji wa Samawah hadi Diwaniyya, kisha wanaenda katika mji wa Hilla kupitia wilaya ya Qassim, au wanaenda hadi Najafu na hatimae wanaenda hadi Karbala, hali kadhalika mazuwaru wa mkoa wa Waasit pado wanaendelea kumiminika katika mkoa wa Baabil.

Hakuna kitu kinacho wasukuma kutoa mali ispokua ni mapenzi ya Hussein (a.s), na mazingira ya kila mtu yanasema:

Labbaika mlinganiaji wa Allah, kama muili wangu haukuitika pale ulipoita, na kutaka kunusuriwa, hakika moyo wangu uliitika na masikio na macho yangu.

Hii ni sehemu ya picha za misafara hiyo..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: