Zaidi ya mahafidh 30 wanahudhuria masomo ya kifikra katika ratiba ya malezi ya idara ya tahfiidh

Maoni katika picha
Idara ya tahfiidh chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendesha ratiba ya masomo ya malezi kwa wanafunzi wanaohifadhi kitabu kitakatifu katika mji wa Karbala.

Katika ratiba hii wameshiriki zaidi ya mahafidh (30), chini ya ukufunzi wa Shekh Ali Rawii mmoja wa walimu wa Maahadi, wanasoma siku moja kila wiki, mkufunzi huchagua aya moja inayozungumzia malezi na akhlaq kisha huifafanua, kwa lengo la kuwajenga vizuri katika kuelewa vizito viwili vitakatifu.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu imeweka ratiba ya kielimu, inayolenga kuhifadhi Qur’ani yote ndani ya muda wa miaka (5 – 6), kiwango cha kuhifadhi kimegawanywa kwa idadi ya miezi, sambamba na ratiba ya kutwalii kila siku, sehemu imetengenezwa vizuri kwa kusoma, kila kitu kinacho hitajika kimewekwa madarasani, sambamba na viyoyozi, chakula na sehemu za kupumzikia.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya vituo vya Majmaa Ilmi lilqurani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kusambaza elimu ya Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwelewa mkubwa wa Qur’ani katika sekta zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: