Riwaya zinaonyesha kuwa Yazidi -laana iwe juu yake- baada ya kumaliza kiu ya kutazama kichwa cha Hussein (a.s) na vichwa vya watu wa nyumbani kwake, aliamuru viwekwe sehemu tatu tofauti:
- - Kwenye mlango wa Qasri lake.
- - Kisha milango ya Damaskas.
- - Kisha kwenye milango ya Masjid Jaamia.
Muqarram anasema: Kisha akatoa kichwa na kukisulubu kwenye mlango wa Qasri yake kwa muda wa siku tatu, Yazidi akaamuru vichwa visulubiwe kwenye milango ya mji na kwenye Jaamia Umawiyya, wakafanya hivyo.
Hindu bint Amru bun Suhail mke wa Yazidi alipoona kichwa kipo juu ya mlango wa nyumba yake na nuru inawaka kwenye kichwa hicho, huku kikivuja damu mbichi na kutoa harufu nzuri, aliingia kwenye majlisi akiwa hajavaa hijabu, akamfuata Yazidi na kusema: Kichwa cha mtoto wa bint wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kinasulubiwa juu ya mlango wa nyumba yetu?! Yazidi akasimama na kumfunika, halafu akamuambia: Nisamehe ewe Hindi, hakika ni fujo za bani Hashim, Ibun Ziyadi kafanya pupa akamuua, Allah amlaani.