Wahudumu wanaofaya kazi za kiufundi katika idara ya mitambo na vyuma chini ya kitengo cha ujenzi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekamilisha kazi ya kujenga daraja maalum la chuma kwa ajili ya kupita mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Ustadh Hassan Abdulhussein kiongozi wa idara ya mitambo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Daraja hili hujengwa kwa muda kila unapokaribia msimu wa ziara ya Arubaini, kwa ajili ya kurahisisha upitaji wa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kurahisisha harakati za mawakibu za kuomboleza zinazo ingia katika malalo hiyo zikitokea upande wa uwanja uliopo katikati ya haram mbili tukufu, bila kuleta msongamano”.
Akaongeza kuwa: “Daraja lipo upande wa kusini magharibi mwa Atabatu Abbasiyya tukufu mkabala na mlango wa Imamu Hassan (a.s), wahudumu wetu huanza mapema kufunga daraja hilo, nalo ni moja ya madaraja matatu ambayo hufungwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa mazuwaru pamoja na mawakibu za waombolezaji”.
Akabainisha kuwa: “Daraja linaupana wa (mita 8), linapande mbili, kila upande unaupana wa (mita 4), kwa ajili ya kwenda na kurudi, urefu wake ni zaidi ya (mita 4), linavipande vya mbao kila kimoja kinaurefu wa (mita 2.40) na upana wa (mita 1.22) vimesimamishwa pembezoni mwa daraja kwa ajili ya kuimarisha usalama wa mazuwaru wakati wanapopita juu ya daraja hilo”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake vyote, kikiwemo kitengo hiki, vimekamilisha maandalizi yote ya lazima kwa ajili ya kupokea mazuwaru watukufu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).