Bendera ndefu zaidi ya Husseini duniani yazunguka malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Malalo mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya leo mwezi (10 Safar 1443h) sawa na tarehe (18 Septemba 2021m), zimezungukwa na bendera ndefu zaidi duniani, ina urefu wa (mita elfu 12), imebebwa na watu wa mkoa wa Diyala kutoka milengo tofauti (Sunni, Shia, Wakurdi na Waturkuman), watu wa tabaka zote pia wameshiriki, askari, watumishi, viongozi wa Dini na wazee wa makabila, chini ya kauli mbiu isemayo (Kutoka Diyala yenye msimamo hadi Karbala ya Shahada na kujitolea).

Jambo hili linafanywa kwa mwaka wa sita mfululizo, hufanywa katika siku kama ya leo kila mwaka, matembezi ya ubebaji wa bendera hiyo yameanzia karibu na ofisi kuu yakapita barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s), hadi kwenye haram takatifu ya Husseini kisha wakaelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Abu Bahari Arnu-Utwi kiongozi wa maukibu ya mwenye mbavu iliyovunjika na msimamizi wa ushonaji wa bendera hiyo amesema: “Jambo hili lilianza miaka sita iliyopita kwa kushona bendera yenye urefu wa (mita 2000) hadi leo zimefika (mita elfu 12), kila mwaka hushonwa katika moja ya miji ya Diyala, makundi yote ya watu kutoka mkoa wa Diyala hushiriki katika kubebwa kwake, ni kielelezo cha umoja wetu katika mambo yanayo muhusu bwana wa mashahidi (a.s), mwaka huu imeshonewa katika mji (mpya wa Shatu)”.

Akaongeza kuwa: “kupitia matembezi haya, hutuma ujumbe kwa walimwengu kuonyesha umoja wa raia wa Iraq na wakazi wa mkoa wa Diyala kwa ujumla, tunaidhibitishia dunia kuwa Hussein (a.s) anatuunganisha, na bendera hii ambayo imeandikwa jina lake takatifu na makundi yote tunatembea chini yake ni ishara ya umoja wa raia wa Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: