Naswiriyya yaaga mazuwaru na kuitikia wito wa Arubaini (shuhudia picha)

Maoni katika picha
Mkoa wa Dhiqaar tangu siku nne zilizopita umeshuhudia misafara mingi ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ambapo kuna watu wengi wanao wasiri katika mkoa huo wakitokea mkoa wa Basra wanao tembea kuelekea mji wa shahada na uaminifu mji mtukufu wa Karbala.

Wakazi wa mji huo, wazee kwa vijana wanaume kwa wanawake wamejitokeza kwa wingi kuhudumia mazuwaru sambamba na kuimarisha ulinzi, kama kawaida yao kila mwaka.

Kilele cha misafara hiyo ni leo, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vinavyotoa huduma vimeenea ndani na nje ya mkoa katika kila njia, walianza mapema kufanya maandalizi ya kuhudumia wapenzi wa Husseini, kazi ambayo wamekua wakiisubiri kwa hamu kubwa.

Ziara ya Imamu Hussein (a.s) haiishi hamu, humuweka mwanaadamu katika ukamilifu wa kiimani pamoja na kuongeza kiwango cha kumtambua Imamu Hussein (a.s), sambamba na kujenga ujasiri wa kupambana na matatizo yanayo weza kutokea katika maisha, hilo ndio aliloashiria Imamu Swadiq (a.s) kwa Ibun Bakiir aliyekua anaeleza khofu na mateso aliyopata wakati anaenda kumzuru Abu Abdillahi (a.s), akamuambia: Hivi haupendi Mwenyezi Mungu akuone ukituhofia?.

Hii ni sehemu ya picha zilizopigwa na kamera ya mtandao wa Alkafeel kutoka kwenye matembezi hayo katika mkoa wa Dhiqaar..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: