Mwaka wa tisa mfululizo.. Maahadi ya Qur’ani tukufu inaendesha mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, imefungua vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru katika mkoa wa Muthanna, harakati hii ni sehemu ya mradi wa Tablighi wa hauza ya Najafu.

Mkuu wa Maahadi Shekh Jawaad Nasrawi amesema: “Kituo cha kwanza cha mradi huu kilifunguliwa katika mji wa mkoa wa Muthanna na kuanza kufundisha usomaji wa Surat Faat-ha, na sura fupi pamoja na nyeradi za swala kwa mazuwaru wanaenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini”, akaongeza kuwa: “Vituo hivi vitawekwa pia katika mji wa Diwaniyya, Baabil, Bagdad, wilaya ya Hindiyya na Karbala tukufu”.

Akasisitiza kuwa: “Mradi huu hufanywa kila mwaka, unalenga kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani, hususan wakati wa mkusanyiko wa mamilioni ya watu wanaokuja kufanya ziara kwa bwana wa mashahidi”. Akaashiria kuwa: “Ukamilifu wa swala unategemea kisomo sahihi, baadhi ya waumini ambao hawajasoma Dini na wazee ndio walengwa wakubwa wa mradi huu”.

Kumbuka kuwa mradi unafanywa kwa mwaka wa tifa mfululizo, zaidi ya watu milioni moja wamenufaika na mradi huu katika mika iliyopita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: