Maukibu wa chuo kikuu cha Alkafeel ni kituo cha kwanza cha Atabatu Abbasiyya kinacho hudumia mazuwaru kutoka upande wa Najafu

Maoni katika picha
Maukibu ya chuo cha Alkafeel chini ya idara ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye mkoa wa Najafu, inahudumia mazuwaru watukufu wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini kwa siku ya tatu mfululizo, maukibu hiyo ni kituo cha kwanza cha Atabatu Abbasiyya tukufu katika upande huo.

Rais wa chuo Dokta Nuris Dahani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maukibu ya chuo chetu ni miongoni mwa mawakibu zinazotoa huduma katika mkoa wa Najafu, inapewa kipaombele sana na Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na huduma inazotoa kwa mazuwaru watukufu”.

Akaongeza kuwa: “Watoa huduma katika maukibu hiyo ni wakufunzi wa chuo kikuu na wanafunzi wao pamoja na watumishi, utawakuta wanashindana katika kuhudumia mazuwaru na huzisubiri siku hizi kwa shauku kubwa, maukibu hugawa chakula kiasi cha sahani (1500) kwa siku, kiwango hicho kinaongezeka kila siku, sambamba na kugawa maji baridi ya kunywa muda wote pamoja na juisi”.

Kumbuka kuwa maukibu ya chuo kikuu cha Alkafeel, ilianzishwa sambamba na kuanzishwa kwa chuo, na ikatumia jina la chuo, imekua ikiboresha huduma zake kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: