Kuweka vizuwizi vya barabarani kwa ajili ya kurahisisha utembeaji wa mazuwaru kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya ujenzi katika kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Atabatu Abbasiyya, wameweka vizuwizi kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu unaoshuhudia msongamano wa watu wakati wa ziara, vitakavyo saidia kuratibu utembeaji wa mazuwaru na kuondoa msongamano unaoweza kutokea.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kufanya vikao vingi na viongozi wa Ataba mbili tukufu, kuhusu kuweka utaratibu utakaodhibiti utembeaji wa mazuwaru kwenye barabara zinazo zunguka uwanja wa katikati ya haram mbili, ukizingatia kuwepo kwa hali ya msongamano, tulikubaliana kuweka vizuwizi vinavyo tenganisha wanaoenda na wanaorudi, tukafanya utafiti wa aina ya vizuwizi vitakavyo faa, ndipo idara ya kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili ikapasisha aina hii, kwani inakidhi haja”.

Akaongeza kuwa: “Kazi hii imeanza kufanywa karibu na msimu wa ziara, vizuwizi hivyo vimetengenezwa ndani ya karakana ya idara, vinaubora mkubwa, vitatumika kugawa kila barabara sehemu mbili, upande wa watu wanaoenda na wanaorudi, ili kurahisisha utembeaji wa mazuwaru na mawakibu za kuomboleza zinazo tumia barabara hizo”.

Akamaliza kwa kusema: “Kupitia vizuwizi hivi tunauhakika wa kuwa na matembezi salama, na mazuwaru watafika sehemu wanazokusudia kwa urahisi, bila kutokea msongamano wala usumbufu, hivyo ndio tulivyo fanya katika ziara iliyopita, lakini hatukutumia aina hii ya vizuwizi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: