Kuweka vituo vya utambuzi wa watoto na wazee wanaokuja kwenye ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha hazina katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maandalizi yake ya ziara ya Arubaini, kinasambaza vituo vya kuwatambua watoto na wazee wenye mahitaji maalum, kwa kuweka utaratibu utakaorahisisha kupatikana kwao pale watakapo potezana na wasimamizi wao, kwenye barabara zinazo ingia Karbala tukufu upande wa Baabil, Bagdad na Najafu.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Abdulghina Mahadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi ya vituo vya utambuzi husaidia utendaji kazi wa vituo vya kuelekeza waliopotea, na tunafanya kazi chini ya kamati moja yenye lengo la kumtambua zaairu sawa awe mtoto au mzee, au hata watu wa kawaida wanaohofiwa kupotea wakati wa ziara, kwa kuweka utaratibu unaorahisisha kupatikana kwao kwa kuandika taarifa zao kwenye vituo vya waliopotelewa”.

Akaongeza kuwa: “Vituo hivi vilianzishwa mwaka (2010) na vimesha toa huduma kwa maelfu ya mazuwaru, kila kituo kina watoa huduma ambao hutoa alama za utambulisho kwa anayetaka, alama hizo ni picha ya muhusika ikiwa na (Jina, makazi, namba ya simu ya baba au mtu aliyenae) na huwekwa kwenye mkono wa zaairu (mtoto au mzee), zamani tulikua tunatoa vitambulisho ambavyo wahusika walikua wanavaa shingoni”.

Akabainisha kuwa: “Tumechapisha na kuandaa alama za utambulisho zaidi ya laki mbili na nusu, sambamba na kuandaa wahudumu zaidi ya (200), kutoka ndani ya watumishi wa kitengo chetu na wahudumu wa kujitolea, wanauzowefu mkubwa wa kufanya kazi hii”.

Kumbuka kuwa huduma hii ilipata mwitikio mkubwa na kupongezwa sana na mazuwaru katika misimu iliyopita, waliwashukuru na kuwapongeza watoa huduma wetu kwa kazi nzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: