Kwa mpangilio mzuri idara ya viatu imeongeza ufanisi katika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya viatu chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeongeza ufanisi katika kuhudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati huu wa msimu ya ziara ya Arubaini.

Kuhusu maandalizi ya idara hiyo tumeongea na kiongozi wake Hussein Abdurabah, amesema: “Tumeanza kutekeleza mkakati tulio andaa kwa ajili ya ziara ya Arubaini, tumepanga kabati za kuweka viatu katika maeneo yote yanayo zunguka haram tukufu, sambamba na kuongeza wahudumu wa kujitolea kutokana na idadi kubwa ya watu wanaotarajiwa kuingia katika Atabatu Abbasiyya ndani ya siku chache zijazo”.

Akaongeza: “Kama ilivyo kawaida katika kila ziara kubwa watumishi wetu hutafuta njia bora ya kuhudumia mazuwaru katika utunzaji wa viatu upande wa wanaume na wanawake, kwa kutumia utaratibu wa namba”.

Akasema: “Watu wote tulio waongeza katika utoaji wa huduma wana uzowefu mkubwa wa kuamiliana na mazuwaru katika matukio kama haya, tumesha wahi kufanya nao kazi kwa mafanikio, kazi yao haiishii kwenye kutunza viatu peke yake, bali wanasaidia kuongoza mazuwaru na kuratibu matembezi yao”, akasema kuwa: “Watafanya kazi pamoja na ndugu zao watumishi wa idara kwa zamu tatu, asubuhi, mchana na usiku”.

Akasisitiza kuwa: “Tumechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, kama vile kuvaa soksi za mikononi, barakoa na kutumia vitakasa mikono muda wote, kwa ajili ya kulinda usalama wetu na usalama wa mazuwaru”.

Tambua kuwa idara ya viatu hufanya kila iwezalo katika kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa Arubainiyya na kufanya ibada ya ziara kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: