Samawa yaitikia wito wa Arubaini na misafara ya wapenzi wa Husseini yamiminika katika mji huo

Maoni katika picha
Mji wa Samawa umeitikia wito wa Arubaini, baada ya misafara ya wapenzi wa Imamu Hussein (a.s), kuwasiri kwa wingi katika mji huo tangu zaidi ya siku mbili zilizo pita, misafara hiyo imeanza kuingia katika mji huo wenye mapenzi makubwa ya Imamu Hussein (a.s) kama ilivyo miji mingine, kupitia wilaya ya Hadhar iliyopo katika mkoa wa Muthanna.

Kwa mujibu wa taarifa ya ripota wa mtandao wa Alkafeel ambae yupo kwenye matembezi hayo amesema: “Misafara imeingia Samawa kupitia njia tatu kuu, ambazo ni Al-Aamu, Siyahi zilizopo pembezoni mwa mto wa Furaat na Sikkatul-Qitwaar, njia zote tatu zinakutana katika mji wa Samawa, wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi kuhudumia mazuwaru, kwanini wasipokewe na kupewa huduma wakati wao ni wageni wa Imamu Hussein (a.s), mabanda ya kutolea huduma, Husseiniyyaat na nyumba za watu wote wamefungua milango kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Samawa ni moja ya njia muhimu za mazuwaru, watu wanaotoka katika miko ya kusini (Basra, Naswiriyya, Misaan) hupitia katika mkoa huo, sambamba na wanao ungana nao miongoni mwa wakazi wa mji huo, misafara huwa mingi kwa zaidi ya siku nne”.

Lengo kuu la huduma zote linabakia kuwa lile lililotajwa katika riwaya, ambalo ni utukufu wa ziara ya Imamu Hussein (a.s), na kuhuisha utiifu na mapenzi kwa Ahlulbait (a.s) na kunusuri Imani yao, haya yapo katika ziara: (Na moyo wangu unajisalimisha kwa moyo wenu, na kufuata amri yenu, nipo tayali kuwanusuru).

Hii ni sehemu ya picha zilizopigwa na kamera ya Alkafeel katika matembezi hayo yalipo wasiri kwenye mji huo..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: