Kuhitimisha semina ya mbinu za kuamiliana na mazuwaru

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imehitimisha moja ya semina zake za kujiandaa na ziara ya Arubaini, iliyokua na anuani isemayo: (Mbinu za kuamiliana na mazuwaru) semina hiyo imefanywa kwa kushirikiana na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu.

Mkufunzi wa semina hiyo alikua ni Mhandisi Muhammad Abdulhussein Saaidiy kutoka kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, ilikua na mada nyingi, miongoni mwa mada hizo ni: (tabia njema, fani za uongeaji na kumridhisha mtu, aina za watu na jinsi ya kuamiliana nao, mbinu za kuamiliana na watu wenye umri mkubwa).

Semina inalenga kupata watoa huduma bora kwa mazuwaru, waliofundishwa mbinu za kuamiliana na watu, ndio maana tunawajengea uwezo wa kuamiliana na mazuwaru, kupitia mafunzo ya vitendo yenye uwezo mkubwa wa kukuza vipaji vyao na kutimiza malengo yao ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru na kuboresha mawasiliano baina yao, kwa kuboresha huduma wanazotoa wakati wa ziara.

Abbasi Maliki kiongozi wa kamati ya mipango katika maukibu ya kitamaduni ambayo ipo katika harakati za jumuiya wakati wa ziara ya Arubaini amesema: “Lengo la semina hii ni kuandaa watoa huduma na kukuza uwezo wao kupitia mafunzo ya vitendo kama sehemu ya kujiandaa kutoa huduma kwenye ziara inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu katika siku ya mwezi ishirini Safar, hivyo tunajenga uwezo wa vijana na kuwaandaa waweze kufikisha ujumbe wa maukibu ya utamaduni kwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) katika msimu wa Arubaini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: