Kazi ya mpangilio inafanywa na idara ya Amanaat katika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya Amanaat chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubaini, wameongeza maeneo mapya ya kutunzia vitu kwenye eneo linalozunguka haram tukufu.

Kiongozi wa idara Yaasin Hashim amesema: “Kama inavyojulikana kazi yetu imejikita katika kutunza amana za mazuwaru, vitu na mabeji, tumeamua kuongeza maeneo mapya katika sehemu inayozunguka uwanja wa haram takatifu, sehemu hizo hazikuwepo katika ziara zilizopita, tulikua na sehemu za kutunza mabeji za nje, hali kadhalika tumeandaa kituo cha kusaidia watu wenye mahitaji maalum, kama vile watu wenye ulemavu, wagonjwa na wazee kwa kuweka viti-mwendo maalum kwa ajili yao, pia kunakituo cha kutoa Abaa za kiislamu (hijabu za kiislamu) kwa mazuwaru wa kike”.

Akaongeza kuwa: “Tumeongeza watoa huduma wa kujitolea wenye uzowefu katika kazi hizi, waliokuwa wameshafanya kazi nasisi katika ziara tofauti, kwa ajili ya kuhakikisha tunatoa huduma bora”.

Akaendelea kusema: “Tunafanya kazi kwa umakini mkubwa, tunatumia namba katika kupokea na kutoa amana, sambamba na kuchukua tahadhari zote kiafya kwa lengo la kulinda usalama wa mazuwaru na wahudumu”.

Akafafanua kuwa: “Siku zijazo tutafungua vituo vingine kwa ajili ya kutunza amana, vyenye uwezo wa kubeba maelfu ya mabeji, ili kuongeza uwezo wa mabanda ya kutunza amana yaliyopo katika maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu, yanayofanya kazi mwaka mzima”.

Akasisitiza kuwa: “Watumishi wetu wanafanya kazi pamoja na wahudumu wa kujitolea muda wote, kupitia zamu tatu, asubuhi, mchana na usiku katika kipindi chote cha ziara ya Arubainiyya”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inazingatia sana kuwa na mpangilio mzuri katika kuhudumia mazuwaru, ili kuwawezesha kufanya ibada ya ziara kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: