Hema la maktaba ya bibi Ummul-Banina (a.s) linahudumia mazuwaru wa kike katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Maktaba ya bibi Ummul-Banina (a.s) chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa huduma kwa mazuwari wa kike wa Arubaini, kuanzia leo asubuni siku ya Jumapili (11 Safar 1443h) sawa na tarehe (19 Septemba 2021m).

Hema la maukibu ya Ummul-Banina (a.s) ya kutoa huduma limejengwa katika chuo kikuu cha Al-Ameed, linatoa huduma tofauti kwa njia ya uhudhuriaji na mtandao, kwa namna ambayo inasaidia kutoa elimu kwa mazuwaru ya kifikra, kitamaduni na kidini.

Shughuli zimeanza kwa kuendesha shindano la (Tunajifunza kutoka kwa Maryamu mkuu a.s), lililo andaliwa na idara ya jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) chini ya maktaba hiyo, pamoja na kutoa zawadi kwa washindi.

Bibi Dalali Kamali Akili muandishi wa jarida hilo amesema: “Shindano linalenga kushajihisha usomaji wa jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s), sambamba na kutafiti maudhui zake na mpangilio wa milango yake, linalenga mabinti wenye umri wa miaka (15) na zaidi, shindano hili limefanywa kwa mara ya kwanza mwaka huu”.

Akaongeza kuwa: “Unaweza kushiriki kwenye shindano kupitia link maalum”.

Kumbuka kuwa huduma zinatolewa na maukibu ya wanawake kuhusu Hussein (a.s), nayo ni maukibu ya kitamaduni na kimalezi kwa wanawake, kila mwaka hutoa huduma za kitamaduni kwa mazuwaru wa kike, katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: