Kuanza hatua ya pili ya mradi wa kusafisha njia za mazuwaru

Maoni katika picha
Kikosi cha mradi wa kusafisha njia za mazuwaru, kimeanza hatua ya pili ya kusafisha njia za (Yaa Hussein) kuanzia Najafu kuelekea Karbala, hatua hii imehusisha usafishaji wa barabara.

Msimamizi wa mradi huo Shekh Hussein Turabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni hatua muhimu katika mradi wetu, ulioanzishwa chini ya maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkakati wake wa kuhudumia mazuwaru wa ziara ya Arubaini, pia kutokana na umuhimu wa kazi hii, inasaidia kulea jamii katika kudumisha usafi”.

Akaongeza kuwa: “Makundi ya kikosi kazi yanayo undwa na watumishi wa idara ya usafi na kituo cha Alqamaru cha habari na Maahadi Turathul-Ambiyaa (a.s) na chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, yamesambaa katika barabara za (Yaa Hussein), kwa ajili ya kufanya usafi na kujenga uwelewa wa kudumisha usafi”.

Kumbuka kuwa Maahadi iligawa kiwango kikubwa cha mifuko ya kutupia taka pamoja na kuweka mapipa ya taka kwenye maukibu zilizopo katika barabara inayoelekea Karbala, katika barabara kuu tatu: (Bagdad – Karbala/ Baabil – Karbala/ Najafu – Karbala), kwa ajili ya kusaidia kuhudumia mazuwaru na kudumisha usafi, chini ya mradi wa usafi unaosimamiwa na Maahadi ya Turathul-Ambiyaa (a.s), chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa mwaka wa nne mfululizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: