Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu yafungua vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Najafu chini ya Majmaa Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imefungua vituo vya kufundisha mazuwaru usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu kwa ushiriki wa walimu wa Qur’ani thelathini, katika maukibu ya Ataba mbili tukufu liyopo barabara ya Najafu – Karbala.

Vituo vya ufundishaji wa Qur’ani, vinafundisha usomaji sahihi wa Surat Fat-ha na sura zingine fupi pamoja na nyeradi za swala, kwa mazuwaru wanaoenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini, sambamba na kujibu maswali na kutoa ufafanuzi mbalimbali, na kugawa vipeperushi vinavyo elezea ziara na mafundisho ya Qur’ani.

Tangu kufunguliwa kwa vituo hivyo vimepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, asilimia kubwa ya wanufaika ni vijana ambao hawajasoma Dini na wazee pamoja na kila mtu asiyeweza kusoma Qur’ani kwa usahihi.

Kumbuka kuwa idadi ya wanufaika wa mradi huu kwenye vituo vya Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Najafu ni zaidi ya elfu kumi na sita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: