Mazuwaru wanapita Muthanna na Diwaniyya yawapokea kupitia mji wa Hamza

Maoni katika picha
Misafara ya mazuwaru inaendelea kumiminika barabarani ikielekea katika mji wa watu huru na kilele cha msimamo Karbala tukufu kufanya ziara ya Arubaini, wameapa kupambana na uchovu wa muili na mazingira ya hali ya hewa, hawachoki wala hawaogopi maadam lengo lao ni kumzuru Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya Arubainiyya.

Ripota wa mtandao wa Alkafeel ambaye yupo katika msafara huo wa (Basra, Naswiriyya na Diwaniyya) hadi Karbala amesema: “Mazuwaru na misafara ya magari alfajiri ya leo Jumanne (13 Safar 1443h), wamevuka kituo cha mwisho katika mkoa wa Muthanna, kilichopo katika mji wa Ramitha, na kuwasiri katika mji wa Diwaniyya baada ya kutembea (kilometa 36), wanaingia kwenye mji huo wakipitia kitongoji cha Hamza upande wa mashariki, baada ya kupita vitongoji vya Aaridhiyaat, Twabu na Abu-Habibaat vilivyopo kwenye barabara inayoelekea katika mji huo”.

Akaongeza kuwa: “Mji wa Diwaniyya unaumaalum wake, ndipo hukutana mazuwaru wanaotoka Basra, Misaan na Muthanna, pamoja na sehemu ya mazuwaru wanaotoka mkoa wa Waasit bila kusahau wanaotoka kwenye vitongoji tofauti vya Diwaniyya, hufika katika mji huo kwa kutumia barabara kubwa na ndogo”.

Akabainisha kuwa: “Idadi ya mazuwaru inaendelea kuongezeka, na huduma mbalimbali zinaendelea kutolewa na mawakibu Husseiniyya pamoja na wakazi, waliofungua roho zao kabla ya nyumba kwa ajili ya kutoa huduma ambazo ulimi hauwezi kueleza wala kalamu kuandika”.

Hakuna kinacho wasukuma kufanya kazi na kutoa mali zao, ispokua mapenzi ya Hussein (a.s), mazingira yao yanasema:

Labbaika Daiya-Llah.. kama muili wangu haukuitikia pale ulipoita kuja kukunusuru, moyo wangu, masikio yangu na macho yangu viliitika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: