Kitengo kinacho hudumia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kimemaliza maandalizi ya ziara ya Arubaini na kimeanza kutekeleza mkakati wake

Maoni katika picha
Watumishi wanaohudumia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, wamekamilisha maandalizi ya ziara tukufu ya Arubaini.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu wameanza kutekeleza mkakati wa kitengo ulioandaliwa kwa ajili ya kufanikisha ziara ya Arubaini, wamejipanga kuweka mazingira tulivu kwa mazuwaru katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, sambamba na kuratibu utembeaji wao”.

Akaongeza kuwa: “Idara ya kutoa huduma inafanya kazi muda wote, inasafisha uwanja na barabara zinazo zunguka eneo hilo wakati wote, inagawa maji kwa mawakibu na mazuwaru muda wote na kuratibu matembezi ya kwenda na kurudi wakati wote”.

Akasema: “Watumishi wa idara ya matangazo wanaongoza matembezi ya mazuwaru ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, sambamba na kuruhusu kila chombo cha Habari kinachopenda kurusha matukio ya ziara kutokea katika uwanja huo”.

Akafafanua kuwa: “Kazi haitaishia katika siku ya (20 Safar), bali tutaendelea na kazi zingine baada ya siku hiyo, zitakazo husisha mji mkongwe wa Karbala tukufu”.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, ni sawa na vitengo vingine, kinafanya kazi kubwa katika kuhudumia mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika ziara ya Arubainiyya inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: