Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Baabil yakamilisha maandalizi ya mradi wa vituo vya Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa-Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha maandalizi ya mradi wa vituo vya Qur’ani.

Kiongozi wa idara ya harakati za Qur’ani Ustadh Nuumani Maamuri amesema: “Vituo vya Qur’ani vitakuwa na walimu zaidi ya (120)” akasema: “Vimewekwa katika barabara zinazo elekea Karbala, ndani ya eneo la makao makuu ya mkoa na mtaa wa Abu Gharqi na barabara ya Hilla/ Diwaniyya, pamoja na kwenye wilaya ya Musayyibu na maeneo yanayo zunguka wilaya hiyo”.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil, linafanya harakati mbalimbali za Qur’ani, pamoja na kuendesha semina za Qur’ani.

Tambua kuwa mradi wa vituo vya Qur’ani unafanywa kwa mwaka wa tisa mfululizo kwenye mikoa tofauti, wakati wa ziara tukufu ya Arubainiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: