Maonyesho ya Qur’ani katika barabara ya mazuwaru

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Najafu chini ya Majmaa Ilmiy Lilqur’anil-Kariim, kwa mwaka wa pili mfululizo inafanya (maonyesho ya Qur’ani katika ziara ya Arubainiyya), nayo ni sehemu ya mkakati wa kuitambulisha Qur’ani tukufu kwa mazuwaru, tunafanya kadri tuwezavyo kumnufaisha zaairu katika hilo, ikiwa ni pamoja na kujenga utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Maonyesho hayo yanafanywa katika maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, yamethibitisha matokeo mazuri na muitikio mkubwa wa mazuwaru, hivyo idara ya Maahadi chini ya maelekezo ya Majmaa imeamua kuongeza huduma na harakati zake.

Maonyesho yana matawi mengi, miongone mwake ni:

  • Tawi la kauli za wanachuoni kuhusu Qur’ani na tafsiri yake.
  • Tawi linaloeleza harakati kuu za Majmaa Ilmiy Lilqur’anil-Kariim na kuzifafanua.
  • Tawi la harakati za Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu na yaliyofanywa kipindi kilichopita na matokeo yake.
  • Tawi la kuonyesha msahafu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, nakala zote, unaozingatiwa kuwa moja ya mafanikio makubwa, ni msahafu wa kwanza kuchapishwa hapa Iraq chini ya raia wa Iraq.
  • Tawi la machapisho ya Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu.
  • Tawi la mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini, nao ni katika miradi yenye mafanikio inayofanywa na Maahadi, kuna mamia ya wanafunzi wa Dini walionufaika.
  • Tawi la kazi za kuonekana, miongoni mwake ni: (Ratiba za Qur’ani, ripoti, usomaji, mihadhara..) na mengineyo.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu hufanya harakati mbalimbali katika kila msimu wa ziara ya Arubaini, harakati za Qur’ani wanazotoa kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kila msimu huongezwa vipengele vingine sambamba na kuongezeka muitikio wa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: