Zaidi ya walimu 120 wanashiriki kwenye mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Zaidi ya walimu 120 wanashiriki kwenye mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru, unaosimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil chini ya Majmaul-Qur’ani tukufu kwa mwaka wa tisa mfululizo.

Walimu wamegawanywa sehemu nane hapa mkoani, kwa ajili ya kufundisha watu wanaoenda Karbala sura fupi na nyeradi za swala.

Mradi huu unahuduma tofauti za Qur’ani kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ikiwa ni pamoja na mashindano ya kuhifadhi Qur’ani, mazuwaru wanapata mafundisho yanayokata kiu yao katika kitabu kitukufu.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil. linafanya harakati mbalimbali za Qur’ani tukufu, sambamba na miradi yake, na miradi ya semina endelevu za Qur’ani hapa mkoani.

Tambua kuwa mradi wa vituo vya Qur’ani unafanywa kwa mwaka wa tifa mfululizo katika Mikio mingi kwenye msimu wa kumbukumbu ya ziara tukufu ya Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: