Diwaniya imejaa mazuwaru wa Arubaini wanaotembea kwenda kibla ya utukufu na uaminifu

Maoni katika picha
Misafara ya mazuwaru inatembea kuelekea Karbala, katika matembezi yasiyokua na mfano duniani, mji wa Diwaniyya asubuhi ya leo siku ya Jumanne, umeshuhudia misafara mikubwa ya mazuwaru iliyo wasiri kutokea mikoa ya kusini, barabara zote vimejaa mazuwaru hao, pamoja na changamoto ya kuongezeka kiwango cha joto lakini misafara inaendelea kumiminika bila kukatika, kwa nini ikatike wakati lengo ni kiini cha uhai na njia ya uhuru!

Ripota wa mtandao wa Alkafeel ambae yupo kwenye matembezi hayo amesema: “Mji huu uliojaa wapenzi wa Hussein (a.s) na mazuwaru wake, wakazi wa mji huu wazee kwa vijana wanawake kwa watoto wanashindana kuhudumia mazuwaru, mawakibu, husseiniyya na nyumba zimefungua milango yao na kutoa kila aina ya huduma inayohitajika, chini ya ulinzi mkali kutoka kwa vikosi vya usalama vya hapa mkoani”.

Akaongeza kuwa: “Mazuwaru wamewasiri kutoka mkoa wa Basra, Naswiriyya, Misaan na sehemu kutoka mkoa wa Waasit, pamoja na baadhi ya maeneo ya mkoa huu bila kujali uchovu na ugumu wa hali ya hewa, japokua nyuso zao zimejaa vumbi lakini utaona nuru kwenye paji zao na uchamungu unao wasukuma kwenda kwa kibla wa watu huru”.

Hawa ndio mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), wanaongozwa na kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Ewe Mola.. zirehemu nyuso zilizobadilika kutokana na jua, na urehemu yale mashavu yanayo geuka geuka kwenye kaburi la Abu Abdillahi Hussein (a.s), na urehemu macho yanayotokwa machozi kutulilia, na urehemu zile nyoyo zilizohuzunika kwa ajili yetu, na urehemu wanaopiga kelele kwa ajili yetu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: