Maukibu ya Ummul-Banina (a.s) inatoa huduma tofauti muda wote

Maoni katika picha
Maukibu ya Ummul-Banina (a.s) iliyopo katika chuo kikuu cha Al-Ameed kwenye barabara ya (Najafu – Karbala), ni maukibu muhimu inayotoa huduma kwa mazuwaru wa ziara ya Arubaini katika barabara hiyo, ilianza kutoa huduma mbalimbali tangu siku za kwanza kumiminika mazuwaru katika barabara hiyo.

Msimamizi wa maukibu hiyo bwana Majidi Muhammad Rabii ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maukibu hii hufikiwa na asilimia kubwa ya mazuwaru wanaoenda Karbala kwa kupitia upande huu, kutokana na kuwepo kwa huduma tofauti, kama chakula milo mitatu kila siku, pamoja na vyakula vyepesi vyepesi, matunda, juisi na maji baridi ya kunywa yanayo tolewa muda wote”.

Akaongeza kuwa: “Maikibu inasehemu mbili: sehemu ya wanaume na sehemu ya wanawake, kila sehemu inatoa huduma ya malazi, chakula, matibabu pamoja na kutoa maelekezo ya kiafya, huduma ya Tablighi ya Dini na huduma za kitamaduni na kimalezi, kunamiradi miwili ya kitamaduni, wa kwanza ni kituo cha utamaduni chini ya idara ya uhusiano na vyuo vikuu na shule, ambapo vinashiriki vitengo kadhaa vya Ataba tukufu, pili ni maukibu ya malezi kwa mabinti (maukibu ya wanawake pembezoni mwa Hussein a.s), inashiriki idara ya wanawake katika Ataba tukufu”.

Akafafanua kuwa: “Maukibu inakituo cha afya cha wanawake na wanaume, na kituo cha kuhudumia waliopotezana na kituo cha utambuzi wa watoto waliopotea”.

Kumbuka kuwa maukibu hii inatokana na umoja wa watoa huduma wa Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao wanasifika kwa kutoa huduma bora kwa wanawake, pamoja na kuwepo katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya, jambo hilo halijaathiri utoaji wa huduma, haijafunga milango yake, bali imeongeza huduma kutokana na usaidizi wa watu na vifaa kutoka chuoni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: