Vituo vya Qur’ani katika mji wa Karbala vyapokea maelfu ya mazuwaru

Maoni katika picha
Vituo vya mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru katika mji mtukufu wa Karbala, unaosimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, vinapokea maelfu ya mazuwaru wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), wanawafundisha usomaji wa surat Fat-ha na sura fupifupi na nyeradi za swala.

Vituo vimewekwa pande kuu za hapa mkoani, kama vile upande wa Najafu, upande wa Baabil, upande wa Bagdad, wasimamizi wa vituo hivyo wamepokea maelfu ya mazuwaru wanaopenda kujifundisha, wengi wao wakiwa ni watoto na watu wasiojua kusoma na kuandika.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu na matawi yake ya mikoani, wanaendesha mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru mwaka wa tisa mfululizo, zaidi ya watu milioni wamesha nufaika na mradi huu katika miaka ya nyuma.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kusambaza elimu ya Dini, ikiwemo “elimu ya Qur’ani” na kuchangia katika kutengeneza jamii yenye uwelewa na uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta zote za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: