Kazi ya kuratibu na kutoa huduma inafanywa na watumishi wa haram katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya kazi kubwa katika ziara ya Arubaini, ili kufanikisha ibada ya ziara, wanasimamia utembeaji wa mazuwaru na utekelezaji wa ibada.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Adnani Quraishi amesema: “Katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu majukumu yetu huongezeka, kitengo chetu husafisha na kutandika mazulia ya ziada pamoja na kupuliza dawa za kuua bakteria na kujikinga na maambukizi ndani ya haram tukufu, hali kadhalika tumeweka idadi kubwa ya vitabu vya ziara na turba”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa majukumu yetu ni kuratibu matembezi ya mazuwaru na kuhakikisha misafara ya kuingia na kutoka inatembea bila kukwama, hivyohivyo upande wa wanawake”.

Akasema kuwa: “Tumeandaa gari za kutumia umeme na tumezigawa makundi mawili, kundi la kwanza kwa ajili ya uokozi, kazi hiyo inafanywa kwa kushirikiana na idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya, kundi la pili zinatumika kwa ajili ya kubeba chakula cha mawakibu za kutoa huduma zilizo chini ya Ataba tukufu upande wa nje”.

Makamo rais wa kitengo cha usimamizi wa haram akafafanua kuwa: “Tuna wahudumu wa kujitolea (750) wenye uzowefu wa kuamiliana na mazuwaru katika tukio kama hili muhimu, wengi wao wamepata uzowefu kupitia kutoa huduma katika siku za Ijumaa ambazo huwa na watu wengi mwaka mzima”.

Tambua kuwa kitengo cha usimamizi wa haram kinamajukumu mengi ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile kudeki, kufagia, kutandika miswala na mangineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: