Msimu wa Arubaini ya Hussein (a.s) unashuhudia harakati nyingi, mawakibu za waombolezaji ni moja ya sehemu muhimu ya maombolezo hayo, malalo takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), Ijumaa ya leo mwezi 16 Safar 1443h) sawa na tarehe (24 Septemba 2021m) mawakibu za zanjiil zimefungua ukurasa mpya katika maombolezo ya Arubaini.
Zimemiminika mawakibu moja baada ya nyingine, zikiwa katika makundi yaliyopangika, matembezi yao yanaanzia sehemu iliyopangwa kwa ajili yao, katika barabara ya kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi ndani ya ukumbi wa haram yake tukufu, wameimba kaswida za kuomboleza zinazo dhihirisha ukubwa wa majonzi waliyonayo katika kumbukumbu ya Arubaini ya bwana wa vijana wa peponi (a.s).
Baada ya hapo wanaelekea katika ukumbi wa haram ya ndugu yake na mbeba bendera wake Abulfadhil Abbasi (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakipiga matam na kulia, baada ya kuwasiri katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mara nyingine tena wanaanza kulia pamoja na kuimba kaswida za kuomboleza na kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwa (a.s).
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu, bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kuwasili kwa mawakibu hizi, zinazo wakilisha asilimia kubwa ya mikoa ya Iraq kutadumu kwa muda wa siku mbili, zitakuja kwa kufuata ratiba kama ilivyo pangwa kuanzia sehemu ya kunzia matembezi hadi mwisho, kwa namna ambayo watatembea kwa urahisi bila kusababisha usumbufu kwa mazuwaru wengine, kwani watatembea ndani ya maeneo waliyo pangiwa”.
Kumbuka kuwa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu, Husseiniyya na Abbasiyya wameweka ratiba ya matembezi ya mawakibu hizo, inayo onyesha sehemu ya kuanzia matembezi na mwisho wa matembezi hayo pamoja na muda wa kila maukibu kwa namna ambayo hazitaingiliana na harakati za mazuwaru.