Kituo cha afya katika mgahawa wa Abulfadhil Abbasi wa mje kinatoa huduma zote za afya

Maoni katika picha
Idara ya Swidiiqah Twahirah (a.s), inayotoa huduma za afya kwa wanawake chini ya idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imefungua vituo vingi vya afya kwa ajili ya kuhudumia wanawake pamoja na kutoa maelekezo kwa mazuwaru wa Arubaini, miongoni mwa vituo vilivyo anza kazi mapema katika siku za kwanza za ziara hii, ni kituo cha mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wa nje, uliopo katika barabara ya Najafu.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Chini ya mkakati wa matibabu uliowekwa na Atabatu Abbasiyya tukufu wakati wa ziara ya Arubaini, idara yetu imechukua jukumu la kuhudumia mazuwaru wa kike, tumeandaa sehemu maalum za kutolea huduma, zinazo endana na mazingira ya afya yaliyopo kwa sasa, miongoni mwa vituo vinavyo toa huduma zote za afya ni kituo hiki cha mgahawa wa nje”.

Akaongeza kuwa: “Kituo hiki kinaumuhimu mkubwa kwani kinatoa huduma zote, kimekua kimbilio kuu la mazuwaru wanaotumia barabara hii, kituo kimejipanga vizuri na kimefanikiwa kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma za afya kwa mazuwaru, chini ya madaktari wa kike mahiri, kituo kinatoa huduma muda wote, kinapokea na kuhudumia wagonjwa walio katika hali yeyote”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mwaka wa pili mfululizo, imeongeza na kuboresha huduma za afya katika maeneo tofauti, kwa mazuwaru wa Arubaini, idara ya madaktari imeandaa mkakati madhubuti kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karbala na mamlaka zingine, ili kuwawezesha kutoa huduma bora, idara ya Swidiqah Twahirah katika ratiba hii inazaidi ya wahudumu wa kujitolea (320) madaktari na wauguzi, ambao tumewagawa kwenye vituo tofauti vya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: