Kazi kubwa inafanywa na wahudumu wa idara ya usafi katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi inafanya kazi kubwa wakati wa msimu wa ziara ya Arubaini, katika kulinda usafi kwenye maeneo yanayo zunguka haram takatifu, wahudumu wake wanafanya kazi saa (24).

Kiongozi wa idara ya usafi bwana Ahmadi Jawadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Safar, maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu yamegawanywa sehemu tatu, sehemu ya kwanza inaanzia katika uwanja mkuu hadi barabara ya Kibla, sehemu ya pili inaanzia katika mlango wa Kibla ya malalo ya Imamu Hussein (a.s) hadi barabara ya Hauraa na sehemu ya tatu inaanzia mlango wa Imamu Ali Haadi (a.s) hadi kwenye barabara ya Atwariin na eneo la katikati ya haram mbili tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Tumeandaa vifaa vyote wanavyo hitaji watumishi wa usafi, ili waweze kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa Arubaini, aidha tumeongeza wahudumu wa kujitolea wapatao (700) wamegawanywa katika zamu mbili: zamu ya kwanza saa (1 asubuhi) hadi saa (1 jioni), na zamu ya pili saa (1 jioni) hadi saa (1 asubuhi)”.

Akasema: “Tumesambaza idadi kubwa ya pipa za kutupia taka, tumeweka pipa (85) katika barabara kuu inayo elekea Atabatu Abbasiyya tukufu na (80) zingine zenye ukubwa tofauti katika eneo linalozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akafafanua kuwa: “Tunashirikiana kukusanya uchafu kati ya idara ya usafi na mawakibu zilizopo katika barabara ya Abbasi, tumegawa idadi kubwa ya mifuko ya kutupia taka kwa mawakibu, ili waweze kudhibiti usafi”.

Kiongozi wa idara ya usafi akasema: “Hali kadhalika tumeandaa sehemu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kulala watoa huduma wa kujitolea waliokuja kuhudumia mazuwaru wa Arubaini kutoka miji tofauti ya Iraq, watumishi wa idara yetu wanatoa huduma zingine pia kwa kushirikiana na vitengo vingine vya Ataba tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: