Kikosi cha daktari wa familia kwa njia ya mtandao chataja huduma zake

Maoni katika picha
Kikosi cha daktari wa familia kwa njia ya mtandao, moja ya miradi ya kituo cha Alqamaru cha Habari chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetaja shughuli zake za kiafya kwa njia ya mtandao katika ziara ya Arubaini.

Jukwaa lao ninaongozwa na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya Iraq, waliobobea katika fani tofauti, wanawake, Watoto, viungo, tumbo na mambo mengine, ikiwa ni pamoja na kufungua ukurasa wa ushauri nasaha, ambapo hujibu kila swali na kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali, kila Daktari hufafanua jambo alilo bobea kwa kiasi ambacho muulizaji hupata majibu yaliyoshiba.

Wahudumu wanafanya kazi kwa kujitolea kulingana na mazingira ya baadhi za familia, aidha hutoa nasaha na maelekezo ya kiafya yanayo endana na kila rika, kuanzia watoto hadi wazee, katika kipindi hiki wanatoa huduma pia kwa mazuwaru wa Arubaini na makundi mengine.

Huduma zote zinatolewa bure na ziko wazi kwa kila mtu, kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii na kwenye facebook ukurasa wa -familia-, na telegram: t.me/OnlineFamilyDr ili kujiunga kwenye grupu tumia link hii: (@Electronicfamilydoctor).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: