Hizi ndio huduma zinazotolewa na majengo ya Shekh Kuleini kwa mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Wahudumu wa jengo la Shekh Kuleini (r.a) chini ya Atbatu Abbasiyya tukufu, wanatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa Arubaini wanaoenda Karbala kwa miguu.

Kiongozi wa majengo hayo bwana Hilali Hamudi Ibrahim amesema: “Mwezi tano Safar tulianza kutoa huduma kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaoenda Karbala kwa miguu, tumegawa maelfu ya sahani za chakula, kuanzia chakula cha asubuhi, mchana na jioni”.

Akaongeza kuwa: “Hatugawi chakula kwa mazuwaru peke yake, bali tunawapa pia mamia ya ndugu zetu wanaojitolea katika kikosi cha Abbasi cha wapiganaji waliosambaa maeneo yote ya Karbala”.

Akasema: “Majengo ya Kuleini yanatoa huduma zingine pia tofauti na chakula, kama vile huduma za afya, sehemu za kupumzika mazuwaru, sehemu za kuswalia. Sehemu za kupumzika na kiswali zimegawanywa sehemu mbili, sehemu ya wanaume na wanawake”.

Hamudi akaendelea kusema: “Kutokana na uzowefu wa wahudumu wetu waliopata kwa kuhudumia mazuwaru miaka mingi, wanaumahiri mkubwa katika kuratibu huduma zao na wanazitoa kwa ustadi mkubwa”.

Kumbuka kuwa majengo ya Shekh Kuleini yapo umbali wa (klm 17) kutoka makao makuu ya mkoa wa Karbala upande wa Bagdad, eneo la majengo hayo linaukubwa wa (2m21.104), yanapande mbili kuu, upande wa kutoa huduma kwa wanaume na upande wa kutoa huduma kwa wanawake, huduma ziko sawa kwa pande zote, nayo ni moja ya sehemu nyingi za kutoa huduma zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, zilizo eneo katika barabara zinazo elekea mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: