Tangazo la ratiba ya kuingia mawakibu za kuomboleza za matam zitakazo shiriki kwenye ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetangaza ratiba ya kuingia kwa mawakibu za kuomboleza za (matam) zinazoshiriki katika Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ya mwaka huu 1443h.

Rais wa kitengo bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Viongozi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kutoka mikoa yote ya Iraq, waheshimu ratiba tunayotoa hivi sasa, ratiba hii inaonyesha muda wa kuondoka kwenye jukwaa lililopo karibu na uwanja wa barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s), kisha kuingia katika Atabatu Husseiniyya kisha kuelekea katika Atabatu Abbasiyya na kumaliza matembezi huko”.

Salmaan amezitaka maukibu: “Kutohalifu ratiba hii kwa ajili ya kumtumikia Imamu Hussein (a.s) na mazuwaru wake, sambamba na kuheshimu kanuni za kujikinga na maambukizi kama zilivyo tolewa na idara ya afya, kila maukibu itapewa nafasi mbili, mara ya kwanza (zanjiil) na mara ya pili (matam), kila moja itaingia kulingana na mkoa wake kwa kuzingatia muda waliopewa, kiongozi wa maukibu atagonga muhiri kuonyesha idadi ya mara alizo ingia”.

Jeduali la ratiba:

18 Safar 1443 hijiriyya:
  • 1- Mkoa wa Dhiqaar wilaya zake na vitongoji vyake, kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.
  • 2- Mkoa wa Misaan wilaya zake na vitongoji vyake, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 kabla ya Adhuhuri.
  • 3- Maukibu ya kuomboleza ya taasisi ya Badri, kuanzia saa 7 Adhuhuri hadi saa 2 Adhuhuri.
  • 4- Mkoa wa Diyala na Swalahu-Dini, kuanzia saa 8 mchana hadi saa 10 Alasiri.
  • 5- Kundi la Answaar Shahidi Swadr, kuanzia saa 10 Alasiri hadi saa 11:30 jioni.
  • 6- Mkoa wa Waasit na wilaya zake na vitongoji vyake, kuanzia saa 1 usiku hadi saa 2 usiku.
  • 7- Mkoa wa Diwaniyya wilaya zake na vitongoji vyake, kuanzia saa 2 usiku hadi saa 4 usiku.
  • 8- Mkoa wa Bagdad wilaya zake na vitongoji vyake, kuanzia saa 4 usiku hadi saa 5 usiku.
  • 9- Mawakibu kutoka nchi za kiarabu na kiislamu, kuanzia saa 5 usiku hadi saa 6 usiku.
19 Safar 1443 hijiriyya:
  • 1- Kadhimiyya takatifu, kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 2 asubuhi.
  • 2- Mkoa wa Najafu wilaya zake na vitongoji vyake, kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.
  • 3- Mkoa wa Basra wilaya zake na vitongoji vyake, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 kabla ya Adhuhuri.
  • 4- Mkoa wa Muthanna wilaya zake na vitongoji vyake, kuanzia saa 7 Adhuhuri hadi saa 2 Adhuhuri.
  • 5- Maukibu ya Hizbu-Da’wah + Kabila la Bani-Tamim, kuanzia saa 8 Adhuhuri hadi saa 10 Alasiri.
  • 6- Mkoa wa Baabil wilaya zake na vitongoji vyake, kuanzia saa 10 Alasiri hadi 11:30 jioni.
  • 7- Mkoa wa Karkuuk na Nainawa, kuanzia saa 1 usiku hadi saa 3 usiku.
  • 8- Wilaya ya Ainu-Tamru, kuanzia saa 3 usiku hadi saa 4 usiku.
  • 9- Mawakibu kutoka nchi za kiarabu na kiislamu, kuanzia saa 4 usiku hadi saa 6 usiku.

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: