Hashdu Atabaat tukufu imefanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Jumamosi jioni Hashdu Atabaat wamefanya mkutano na waandishi wa habari katika mkoa wa Karbala kuhusu ziara ya Arubaini, mkuu wa mkoa wa Karbala ameshiriki katika mkutano huo.

Viongozi wa vikosi vya Hashdu Atabaat wameonyesha ushiriki wao kwa kusaidiana na jeshi la serikali katika kulinda mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubaini sambamba na kutoa huduma zingine.

Mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Khatwabi, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na vikosi hivyo ya kulinda mazuwaru na kuwahudumia, aidha amewashukuru wakazi wa Karbala kwa ushirikiano mzuri wanaotoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama, na kuviwezesha kutekeleza mkakati wa kuimarisha ulinzi kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: