Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imefungua vituo vya Qur’ani kwa mazuwaru wakike

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imefungua vituo kwa kufundisha na kusahihisha usomaji wa surat Fat-hah na sura fupi, pamoja na kubainisha vitendo vya swala na hukumu za kifiqhi kwa mazuwaru wa kike wanaoenda kufanya ziara ya Arubaini.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huduma za mradi wa vituo vya Qur’ani vilivyopo kwenye barabara zote zinazoelekea Karbala hazijaishia kwa wanaume peke yake, bali kuna harakati za Qur’ani kwa wanawake pia, kupitia wahudumu wa kike waliopo kwenye vituo vilivyo wekwa kwenye barabara zinazotumiwa na mazuwaru.

Akaongeza kuwa: “Vituo hivi vinalenga kuhamasisha nafasi ya Qur’ani katika matembezi ya Husseiniyya, sambamba na kutoa nafasi kwa mazuwaru wengi zaidi kunufaika na ratiba hii, wahudumu wetu wanafundisha usomaji wa surat Fat-hah kwa njia sahihi, kutokana na umuhimu wa sura hiyo katika Maisha ya muislamu ukizingatia kuwa nguzo muhimu katika swala, wanafundisha pia vitendo vya swala na nguzo zake pamoja na kujibu maswali ya mazuwaru, yanayohusu mambo mawili makuu tuliyotaja sambamba na kubainisha hukumu za kifiqhi kwa mazuwaru wa kike”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake ilichagua wasomi wa kike na kuwaandaa kwa ajili ya mradi huu, unaoenda sambamba na mradi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu upande wa wanaume.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: