Muhimu: Ziara ya Arubaini kwa niaba ya kila aliyepata udhuru wa kuja kuifanya

Maoni katika picha
Idara ya teknolojia na taaluma za mitandao chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inatangaza kufungua mlango wa kujisajili kufanyiwa ziara ya Arubaini, kwa niaba ya kila aliyepata udhuru wa kuja kufanya ziara hiyo kutoka ndani au nje ya Iraq, usajili unafanywa katika ukurasa wa ziara kwa niaba, uliopo kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel, ambao ni mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ziara hizo zitafanywa na wahudumu wa malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambao ni Masayyid pamoja na wahudumu wengine, kwa niaba ya wapenzi wote wa Ahlulbait (a.s) dunia nzima, wale ambao wameshindwa kuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini kutokana na mazingira ya sasa.

Mlango wa kujisajili ulifunguliwa kupitia ukurasa wa ziara kwa niaba siku kumi kabla ya siku ya ziara, ili kutoa nafasi ya kujisajili watu wengi zaidi kupitia mitandao yote iliyo chini yetu, ibada ya ziara maalum ya Arubaini, swala ya ziara na dua, vitafanywa ndani ya haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwaniaba ya kila mtu atakaejisajili.

Kumbuka kuwa huduma ya ziara kwa niaba kupitia ukurasa wa mtandao wa Alkafeel, hutolewa katika kila ziara maalumu, zikiongozwa na ziara ya Arubaini, idara inayofanya ziara hizo inaipa umuhimu maalum kwa ziara hii inayofanywa kwa mwaka wa pili mfululizo ambao idadi kubwa ya watu wanashindwa kuja kufanya ziara kutoka ndani na nje ya Iraq, kwa sababu ya mazingira ya afya yaliyosababisha nchi nyingi kufunga mipaka yao na kuweka vikwazo vya safari kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: