Njia ya kumpata aliyepotea katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kamati inayosimamia vituo vya kuelekeza waliopotea, imetangaza njia za kumpata aliyepotea, sawa awe mtoto, mzee au mgonjwa.

Kamati imesema kuwa njia ya kwanza ni kuwasiliana na moja ya vituo vya kuelekeza waliopotea, vilivyopo katika kila barabara inayoelekea Karbala pamoja na makao makuu ya mji, na kuwapa jina la mtu aliyepotea na wasifu wake na taarifa zingine zinazo weza kuwasaidia kutoa msaada, kituo kitaangalia taarifa walizo nazo, ambazo zipo kwenye kila kituo.

Kama wasipo muona -Allah aepushe hilo- wataingiza taarifa hiyo na itaonekana kwenye vituo vyote na kwenye vituo vya ukaguzi, kupitia program maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo sambamba na mawasiliano ya moja kwa moja baina ya vituo, kama asipopatikana baada ya hatua hiyo, watachukua namba ya simu ya mtu aliyepotelewa kwa ajili ya kumpitia wakati wowote baada ya kupatikana aliyepotea ili aende kumchukua, kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu ya bure kwa namba (174).

Mradi huu unahusisha pia ufunguaji wa vituo vya kulala watu waliopotea katika maeneo yote, vyenye huduma zote anazohitaji mwanaadamu, sawa awe mtoto au mzee, hadi ndugu yake atakapokuja kumchukua, pia tunagari zinazosaidia kubeba waliopotea kuwatoa kituo kimoja hadi kingine.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu ni mdau mkuu katika kuongoza waliopotea, jumla ya vituo (40) vinashiriki katika zoezi hili kwa kushirikiana na vitengo na idara tofauti, maka vile: (mawasiliano – hazina – Habari – usimamizi wa majengo ya kihandisi – utumishi), idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule imetoa wanafunzi (350) cha chuo, wanaojitolea kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya idara hiyo, mradi huu ni sehemu ya mkakati wa kuhudumia mazuwaru wa Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: