Mawakibu za kuomboleza (matam) zimeanza uombolezaji wake

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo siku ya Jumapili (18 Safar 1443h) sawa na tarehe (26 Septemba 2021m), mawakibu za kuomboleza Arubaini ya Imamu Hussein (matam), zimeanza kumiminika katika haram mbili takatifu baada ya kumaliza kufanya hivyo mawakibu za (zanjiil) ndani ya siku mbili zilizopita.

Uombolezaji wa mawakibu za (matam) utafanyika kwa siku mbili pia, kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, inayohakikisha kutokuwepo msongamano wa mazuwaru kuanzia mwanzo wa matembezi hadi mwisho.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mawakibu za kuomboleza zinaanza matembezi yake katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi kwenye haram yake takatifu, halafu zinaelekea katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kama inavyo onyesha kwenye ratiba iliyotolewa kwa kila maukibu”.

Akaendelea kusema: “Harakati za maukibu zitaendelea kwa muda wa siku mbili, zitashiriki maukibu kutoka ndani na nje ya Iraq, maukibu zote zinaomboleza kwa kufuata ratiba iliyopangwa na kitengo chetu, chini ya usimamizi wa moja kwa moja kutoka kwa watumishi wa kitengo chetu na wahudumu wa kujitolea, wanaosimamia matembezi kuanzia mwanzo hadi mwisho, kwa ajili ya kuondoa usumbufu kwa mazuwaru na kuepusha msongamano”.

Makundi ya waumini yamejitokeza wakati wa matembezi ya kuomboleza yaliyowatokea mateka wa Imamu Hussein (a.s), katika siku kama hizi mwaka wa 61 hijiriyya, wamelia na kujipiga vifua huku wakiimba kaswida za huzuni na kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: