Vituo vya ufundishaji wa Qur’ani tukufu katika mji wa Hindiyya vyapokea maelfu ya mazuwaru

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya, limepokea maelfu ya mazuwaru wanaenda kuhuisha ziara ya Arubaini, kupitia vituo kumi na nane vilivyo pande tatu.

Tawi la vituo vya ufundishaji wa usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru, linawalimu themanini wanaoshiriki kwenye ratiba hiyo, wamepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru huku walimu nao wakiwapokea kwa bashasha na kuwahudumia, kwa kusahihisha usomaji wa surat Fat-ha na sura zingine fupi pamoja na nyeradi za swala.

Vituo vinafundisha maarifa ya Qur’ani sambamba na mafundisho ya vizito viwili, kupitia mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa Qar’ani na matawi yake ya mikoani, inatoa huduma za Qur’ani katika mkoa wa Bagdadi, Muthanna, Diwaniyya, Baabil, Hindiyya na Karbala tukufu, chini ya mradi wa ufundishaji wa usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru, ambao wamekua na muitikio mkubwa sambamba na kusifu huduma hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: