Kuanza kukusanya maoni kwa njia ya mtandao kuhusu huduma zinazo tolewa na Ataba mbili tukufu

Maoni katika picha
Kituo cha kimataifa Al-Ameed cha tafiti na masomo, chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinakusanya maoni kwa njia ya mtandao kuhusu huduma zinazotolewa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika ziara ya Arubaini na kuridhika kwa mazuwaru kutokana na huduma hizo.

Kwa ajili ya kutambua changamoto au mapungufu na kutafuta njia ya kutatua au kurekebisha katika msimu mwingine wa ziara, sambamba na kutumiwa kama kielelezo kielimu kinacho weza kutumiwa katika kuandaa masomo yajayo, maoni hayo yanakusanywa kwa kutumia dodoso.

Kituo kinaomba washiriki wajaze kwa umakini, hasa katika kujibu maswali yaliyopo kwenye dodoso hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: