Bendera ya kubba la malalo ya Ridhwawiyya takatifu yafika katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu na msimamizi wa mgahawa (mudhifu) wa nje katika barabara ya Najafu / Karbala Ustadh Jawadi Hasanawi, amepokea ugeni kutoka Atabatu Ridhwawiyya ukiwa na bendera ya kubba la Imamu Ridhwa (a.s).

Ugeni huo ni watumishi wa malalo ya Ridhwawiyya, shughuli ya kukabidhi bendera imepambwa na tenzi za Husseiniyya, ninazo eleza msiba wa Imamu Hussein (a.s) na yaliyojiri kwa familia yake katika siku kama hizi mwaka 61 hijiriyya, pamoja na kaswida za kimashairi zinazo pongeza kazi kubwa inayofanywa na raia wa Iraq katika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini, namna wanavyo jitolea kwa hali na mali katika kuhudumia mazuwaru kwenye ziara hii tukufu, jambo hili linaonyesha mafungamano makubwa yaliyopo baina yao na Imamu Hussein (a.s).

Baada ya hapo wakakabidhi bendera tukufu iliyokua juu ya kubba la Ridhwawiyya, watumishi wa mgahawa na na watu wanaotembea katika barabara ya (Yaa Hussein) wakapata nafasi ya kushiriki kubeba bendera hiyo takatifu na kutabaruku nayo.

Mwisho wa shughuli hiyo Hasanawi alitoa salam na kuwashukuru watumishi wote wa Atabatu Ridhwawiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: